Jifunze Biashara na Ujasiriamali

Biashara, Ujasiriamali

MALENGO YENYE TIJA KATIKA BIASHARA YAKO.

Malengo ni matokeo maalum ambayo mtu hutegemea kupata baada ya kipindi fulani. Mfano kuanzisha biashara yenye kuingiza faida ya shilingi 200,000 kwa mwezi, kununua kiwanja chenye thamani ya shilingi 10,000,000. Malengo yanaweza kuwa ya biashara binafsi, yanaweza kuwa ya biashara ambazo watu wameingia ubia au kampuni.

Mara nyingi tumekuwa tukichanganya katika matumizi neno malengo, mipango na kusudi lakini ukichunguza maneno hayo utagundua yana utofauti mkubwa .
Kusudi husaidia kueleza sababu za kuanzisha biashara wakati malengo ni matokeo maalum kuhusu hiyo biashara na mpango ni namna ya utekelezaji ilikufikia malengo na kutimiza kusudi.
Mfano Kusudi la kuanzisha biashara ni kuongeza kipato wakati malengo yako ni kuanzisha biashara yenye faida ya shilingi 200,000 kwa juma na mpango ni namna ya kutumia rasilimali ulizonazo ili kutengeneza faida ya 200,000 kwa juma na kisha kujiongezea kipato.
Malengo hutofautiana kutoka kwa mtu mmoja kwenda mtu mwingine kwasababu kila mtu ana kusudi lake maalum na wito wa tofauti katika kila  biashara ambayo mtu anafanya. Malengo ndiyo yanayosaidia kuongeza kasi ya kufikia kusudi.
Ni vema ukawa na malengo yatakayotoa mchango chanya katika kufikia  hatima yako kwenye biashara, mahusiano, katika kipawa ambacho Mungu ameweka ndani yako. Malengo hutusaidia kujua ni wapi pakuwekeza muda wetu , wapi pakuwekeza nguvu zetu na wapi pakuwekeza fedha zetu ili tuweze kutimiza kusudi la jambo fulani katika maisha yetu.
Ni vema ukajifahamu kwa kina wewe ni nani ili uweze kuweka malengo stahiki katika biashara yako, ni jambo la ajabu kama wewe malengo yako ni kuwa mwandishi mkubwa katika hiki kizazi na mpaka sasa hujachukua hatua yoyote ya kujifunza kuhusu uandishi na kufanyia kazi yale uliyojifunza, ni jambo la ajabu kama una malengo ya kuwa na biashara kubwa yenye faida ya 500,000,000 kwa mwezi lakini haufanyi tafititi za kiabiashara, hausomi vitabu vya biashara na haujaanzisha biashara ndogo ikiwa ni sehemu ya kujifunza kwa vitendo.
Maisha yasiyokuwa na malengo ni aina ya maisha yenye kiwango cha juu cha utumwa kasababu malengo ndiyo yanakuwekea mipaka ni mambo gani ufanye na ni mambo gani usifanye lakini kama hautakuwa na malengo utafanya kila unachoambiwa kufanya, utakwenda kila sehemu unayoambiwa twende na hatimaye kuwa busy bila tija.
Malengo yanaweza kubadilika zifuatazo ni kati ya sababu ambazo zinaweka kupelekea kubadili lengo/malengo au kuanzisha lengo jipya.
I Kama umegundua hilo lengo haliwezi kukusaidia kutimiza kusudi lako au kufikia hatima yako unaweza kubadilisha lakini yakupasa kufanya tathimi ya kina kabla ya kuchukua hatua ya kuweka lengo lingine.
II Ukifanikiwa kutumiza malengo unaweza kijiwekea malengo mengine lakini yakupasa kuhakikisha unaendelea vizuri kumantain hayo malengo kama ni ya muendelezo mfano kama ulikuwa unalengo la kusoma vitabu 2 kwa juma kwa kipindi cha mwaka mzima ni vema ukaendelea kusoma hivyo vitabu baada ya juma la kwanza, lapili na mpaka mwaka utakapoishi. Usipunguzi kasi wakati bado haujamaliza mwendo kimbia kwa kasi ile mpaka kwenye ending mark yako ya malengo.
Kuwa makini katika kuweka malengo kwasababu usipo yaweka vizuri unaweza kupoteza MUDA wako na FEDHA nyingi katika maisha yako, unaweza kuishi muda mrefu katika maisha yako bila kufanya jambo la maana ambalo litaacha kumbukumbu ya kuwa Mr or Mrs fulani aliwahi kutoa mchango chanya katika jamii.
Napenda kutoa wito kwa kila asomaye makala hii kuweka malengo katika maisha yake na kuyafanyia kazi hayo malengo kwa uaminifu ili afike katika kilele cha mafanikio.
NB : KWENYE BIASHARA TUNATAZAMA MAMBO KATIKA NAMNA YA KUTUSAIDIA KUONGEZA THAMANI NA KUTENGENEZA FEDHA HIVYO MUKTADHA WA  MAKALA  HII UONE THAMANI YA KUWEKA MALENGO
Indelea kutembelea tovuti hii kwa makala zaidia lakini unaweza kujisajili kupiti barua pepe yako ili uweze kupata makala mpya kila tunapoweka.

Jiunge Upokee Makala Zetu kwa Email

2 Comments

  1. Juliana

    Asante sana kwa somo zuri

Leave a Reply